Posts

WADAU WA SEKTA YA ELIMU WATAKA MASOMO YA SANAA SHULENI, WATOTO WAPEWA ELIMU KWA VITENDO

Image
Na Gladness Kowero Arusha. Elimu ya nadharia pekee imeelezwa kuwa changamoto kwa wanafunzi katika kukuza ujuzi wa vitendo, huku wadau wa elimu wakihimiza kuwepo kwa programu zinazowawezesha watoto kujifunza kwa vitendo. Akizungumza mara baada ya  mradi wa kuwafundisha wanafunzi kutengeneza na kutumia vyombo vya muziki kufika shuleni hapo, Mwalimu wa michezo shule ya msingi Arusha School Madamu Adeline Mollel amesema mafunzo hayo yamewasaidia watoto kuelewa zaidi kwa kuwa wamepata nafasi ya kuona na kufanya kile wanachojifunza. “Changamoto kubwa ni kwamba mara nyingi tunapata elimu ya nadharia, lakini kwenye vitendo inakuwa changamoto. Mradi huu umewasaidia watoto kutoka kwenye nadharia na kujifunza moja kwa moja kwa vitendo.”    Mradi huo unaotekelezwa na Warriors from the East kupitia Nile Blues Project, umelenga kukuza vipaji na ubunifu wa wanafunzi, pamoja na kuwafundisha namna ya kutengeneza na kutumia vyombo vya muziki vya asili vilivyotumiwa na mababu zetu. Kwa u...

SHULE YA ST. PATRICK YAUNGA MKONO ELIMU YA AMALI KWA VITENDO.

Image
Shule ya St. Patrick jijini Arusha imeunga mkono Mradi wa Nile Blues unaolenga kuwafundisha wanafunzi utengenezaji na upigaji wa vyombo vya muziki vya asili, kwa lengo la kuhifadhi tamaduni na sanaa za jadi, huku vijana wakijengewa ujuzi wa vitendo na fursa za kujiajiri. Mwalimu mkuu  wa shule hiyo Bwan Mathew Emanuel amesema uongozi wa shule hiyo unaunga mkono elimu ya amali na kuwapa wanafunzi fursa ya kujifunza ujuzi wa vitendo. “Tumepata ushirikiano kutoka Serikali na kibali cha kwenda mashuleni kuwafundisha watoto. Tunawalenga kuwapa ujuzi wa kutengeneza na kutumia vyombo vya asili, kujenga vipaji na kujiamini, lakini pia kuwaandaa kwa fursa za kujiajiri hapo baadaye.” Mradi huo unaoendeshwa na kikundi cha sanaa cha Warriors from the East, umeanzishwa rasmi jijini Arusha na unalenga kuwafikia wanafunzi katika shule kumi, zikiwemo shule tano za msingi na tano za sekondari. Akielezea lengo la mradi huo, mwanzilishi wa Warriors from the East, Bwn. Lwanda Magere, amesema wanafu...

SHULE ZANUFAIKA NA PROGRAMU YA KUJENGA UWEZO WA VIJANA KATIKA MAWASILIANO.

Image
 Na Gladness Kowero Arusha  Katika zama ambazo uwezo wa kuwasilisha mawazo, kujenga hoja na kufanya maamuzi sahihi unatajwa kuwa nguzo muhimu kwa viongozi wa kesho, programu ya Pan African Speech and Debate Dialogue imeibuka kuwa jukwaa linalowajengea wanafunzi ujasiri wa kuzungumza, kufikiri kwa kina na kushiriki mijadala yenye kuleta suluhisho kwa changamoto za Afrika. Hayo yameelezwa na Mwanzilishi wa programu hiyo na Mwalimu shule ya sekondari Butimba kutoka Mwanza ,Godlove Shami, jijini Arusha wakati wa kuhitimisha mdahalo huo na kusema kuwa kupitia programu hiyo, vijana wanapata nafasi ya kujifunza namna ya kujenga hoja, kusikiliza mitazamo tofauti na kujiandaa kuwa viongozi watakaoweza kukabiliana na changamoto za kizazi cha sasa. Kwa upande wa washirika kutoka Marekani akiwemo,Adam Thane [Coordinator in north America for pan African] amesema lengo kubwa la ushirikiano huo ni kuwasaidia vijana kuondokana na hofu ya kuzungumza mbele ya hadhara na kuwapa ujuzi wa mawasili...

NGORONGORO, SIMBA SC WAUNGANA KUITANGAZA TANZANIA DUNIANI KUPITIA UTALII NA MPIRA

Image
  ARUSHA –  Na Gladness Kowero  Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) na Klabu ya Simba SC zimezindua ushirikiano wa kimkakati utakaotumia nguvu ya mpira wa miguu kuitangaza Tanzania kama kitovu cha utalii duniani kupitia kampeni maalumu ya "Simba Visit Ngorongoro – The Pride Returns Home." Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA, Abdul-Razaq Badru amesema ushirikiano huo unaunganisha sekta mbili zenye mchango mkubwa katika uchumi wa taifa, utalii na michezo, kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ya nchi. Badru amesema Simba ni moja ya chapa kubwa zaidi katika soka la Afrika Mashariki na Kati, huku Ngorongoro ikiwa moja ya vivutio vinavyotambulika duniani kutokana na urithi wake wa kipekee na hadhi yake ya kimataifa. Amesema kampeni ya "The Pride Returns Home" itakuwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 90 ya Klabu ya Simba na itasaidia kuhamasisha Watanzania na wageni kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro, huku mapato yatok...

KAYOMBO APATA SIFA KWA KUSUKUMA MAENDELEO ARUSHA.

Image
  Na Mwandishi wetu Arusha  Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, John L. Kayombo, amepata pongezi kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang'onda, kwa usimamizi wa miradi ya maendeleo na juhudi za kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo jijini Arusha, Mwang'onda alisema mafanikio yanayoonekana katika jiji hilo yametokana na uongozi makini, uwajibikaji na ushirikiano kati ya viongozi na watendaji wa halmashauri. Amesema Kayombo anapaswa kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi kwa bidii, uadilifu na ubunifu ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuharakisha maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi. Pia amewataka viongozi na watumishi wa umma nchini kuiga mfano wa Jiji la Arusha kwa kusimamia miradi ya maendeleo kwa uwazi, ufanisi na uwajibikaji, akisema utendaji bora ndio msingi wa kuwaletea wananchi maendeleo endelevu. Mwisho. 

MWANG'ONDA" ARUSHA YAWEKA MFANO KWA MAJIJI MENGINE"

Image
  Na Mwandishi Wetu Arusha  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang'onda, amesema Jiji la Arusha limeweka mfano kwa majiji mengine nchini kutokana na mafanikio yake katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli za kiuchumi na kijamii. Akizungumza wakati wa ziara ya Mbio za Mwenge wa Uhuru jijini Arusha, Mwang'onda alisema mafanikio yanayopatikana katika jiji hilo yanaonyesha uongozi madhubuti na usimamizi mzuri wa rasilimali za umma, hali inayochangia kuboresha huduma na kuinua ustawi wa wananchi. Amesema pamoja na Tanzania kuwa na majiji mengi, Arusha limeendelea kujitofautisha kwa utekelezaji wa miradi yenye matokeo chanya kwa wananchi.  Amezipa pongezi mamlaka za Jiji la Arusha na kuzitaka halmashauri nyingine nchini kujifunza na kuiga mbinu zinazotumika katika kusukuma mbele agenda ya maendeleo endelevu. Mwisho. 

JIJI LA ARUSHA LAVUKA LENGO LA USAJILI WA VIKUNDI VYA PPRA

Image
Na Mwandishi wetu Arusha  Jiji la Arusha limevuka lengo la Serikali la kusajili vikundi vya Ununuzi wa Umma (PPRA) baada ya kusajili vikundi 306, zaidi ya mara mbili ya lengo la vikundi 150 kwa kila halmashauri. Kupitia vikundi hivyo, zabuni zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5.3 zimetolewa, hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kushiriki moja kwa moja katika fursa za zabuni za Serikali. Mafanikio hayo yamebainishwa wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026, ambapo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Wazo Michael Mwang'onda, alipokea taarifa ya utekelezaji na kuipongeza Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kuvuka malengo yaliyowekwa na Serikali. Amesema hatua hiyo inaonyesha usimamizi mzuri na utekelezaji wenye tija wa mpango wa kuwawezesha wananchi kushiriki katika ununuzi wa umma. Mwang'onda amesema mafanikio hayo yanaendana na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha wananchi wanapata fursa sawa za kushiriki ...