KAYOMBO APATA SIFA KWA KUSUKUMA MAENDELEO ARUSHA.
Na Mwandishi wetu Arusha
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, John L. Kayombo, amepata pongezi kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang'onda, kwa usimamizi wa miradi ya maendeleo na juhudi za kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo jijini Arusha, Mwang'onda alisema mafanikio yanayoonekana katika jiji hilo yametokana na uongozi makini, uwajibikaji na ushirikiano kati ya viongozi na watendaji wa halmashauri.
Amesema Kayombo anapaswa kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi kwa bidii, uadilifu na ubunifu ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuharakisha maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi.
Pia amewataka viongozi na watumishi wa umma nchini kuiga mfano wa Jiji la Arusha kwa kusimamia miradi ya maendeleo kwa uwazi, ufanisi na uwajibikaji, akisema utendaji bora ndio msingi wa kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Mwisho.



Comments
Post a Comment