Posts

Showing posts from April, 2026

WATUMISHI NGORONGORO KUNUFAIKA NA MILIONI 500, WAONYWA MIKOPO KAUSHA DAMU.

Image
  NGORONGORO.  Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro imetenga Sh milioni 500 kwa ajili ya watumishi wa umma, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuwainua kiuchumi watumishi wa kada zote. Akikabidhi mikopo hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Murtallah Sadick Mbilu, amesema lengo la mpango huo ni kuwasaidia watumishi kujikwamua na changamoto za kifedha na kuboresha maisha yao. Amesema mikopo hiyo pia inalenga kupunguza utegemezi wa mikopo isiyo rasmi yenye riba kubwa maarufu kama kausha damu. Mbilu amewataka watumishi kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili iwe na tija kwao binafsi na katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi. Aidha, amesisitiza kuwa utoaji wa mikopo hiyo utafanyika kupitia mfumo rasmi wa watumishi ili kuhakikisha uwazi, usawa na kuepusha mgongano wa maslahi. Ameongeza kuwa utekelezaji mzuri wa mpango huo utachangia kuongeza ufanisi wa watumishi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.