MWANG'ONDA" ARUSHA YAWEKA MFANO KWA MAJIJI MENGINE"

 


Na Mwandishi Wetu Arusha 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang'onda, amesema Jiji la Arusha limeweka mfano kwa majiji mengine nchini kutokana na mafanikio yake katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli za kiuchumi na kijamii.


Akizungumza wakati wa ziara ya Mbio za Mwenge wa Uhuru jijini Arusha, Mwang'onda alisema mafanikio yanayopatikana katika jiji hilo yanaonyesha uongozi madhubuti na usimamizi mzuri wa rasilimali za umma, hali inayochangia kuboresha huduma na kuinua ustawi wa wananchi.



Amesema pamoja na Tanzania kuwa na majiji mengi, Arusha limeendelea kujitofautisha kwa utekelezaji wa miradi yenye matokeo chanya kwa wananchi.


 Amezipa pongezi mamlaka za Jiji la Arusha na kuzitaka halmashauri nyingine nchini kujifunza na kuiga mbinu zinazotumika katika kusukuma mbele agenda ya maendeleo endelevu.

Mwisho. 

Comments

Popular posts from this blog

WATUMISHI NGORONGORO KUNUFAIKA NA MILIONI 500, WAONYWA MIKOPO KAUSHA DAMU.

UGANDA ELECTION COMMISSION CONTINUES RECEIVING RESULTS AS MUSEVENI TAKES EARLY LEAD

WANANCHI WA NGORONGORO WAIBUA WASIWASI KUHUSU MAPENDEKEZO YA TUME.