JIJI LA ARUSHA LAVUKA LENGO LA USAJILI WA VIKUNDI VYA PPRA



Na Mwandishi wetu Arusha 

Jiji la Arusha limevuka lengo la Serikali la kusajili vikundi vya Ununuzi wa Umma (PPRA) baada ya kusajili vikundi 306, zaidi ya mara mbili ya lengo la vikundi 150 kwa kila halmashauri. Kupitia vikundi hivyo, zabuni zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5.3 zimetolewa, hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kushiriki moja kwa moja katika fursa za zabuni za Serikali.


Mafanikio hayo yamebainishwa wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026, ambapo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Wazo Michael Mwang'onda, alipokea taarifa ya utekelezaji na kuipongeza Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kuvuka malengo yaliyowekwa na Serikali. Amesema hatua hiyo inaonyesha usimamizi mzuri na utekelezaji wenye tija wa mpango wa kuwawezesha wananchi kushiriki katika ununuzi wa umma.


Mwang'onda amesema mafanikio hayo yanaendana na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha wananchi wanapata fursa sawa za kushiriki katika shughuli za kiuchumi na kunufaika na miradi ya maendeleo. Ameutaka uongozi wa Jiji la Arusha kuendelea kusimamia uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi ili mafanikio hayo yaendelee kuleta manufaa kwa wananchi na kuchochea maendeleo ya taifa.


Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

WATUMISHI NGORONGORO KUNUFAIKA NA MILIONI 500, WAONYWA MIKOPO KAUSHA DAMU.

UGANDA ELECTION COMMISSION CONTINUES RECEIVING RESULTS AS MUSEVENI TAKES EARLY LEAD

WANANCHI WA NGORONGORO WAIBUA WASIWASI KUHUSU MAPENDEKEZO YA TUME.