SHULE YA ST. PATRICK YAUNGA MKONO ELIMU YA AMALI KWA VITENDO.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bwan Mathew Emanuel amesema uongozi wa shule hiyo unaunga mkono elimu ya amali na kuwapa wanafunzi fursa ya kujifunza ujuzi wa vitendo.
“Tumepata ushirikiano kutoka Serikali na kibali cha kwenda mashuleni kuwafundisha watoto. Tunawalenga kuwapa ujuzi wa kutengeneza na kutumia vyombo vya asili, kujenga vipaji na kujiamini, lakini pia kuwaandaa kwa fursa za kujiajiri hapo baadaye.”
Mradi huo unaoendeshwa na kikundi cha sanaa cha Warriors from the East, umeanzishwa rasmi jijini Arusha na unalenga kuwafikia wanafunzi katika shule kumi, zikiwemo shule tano za msingi na tano za sekondari.
Akielezea lengo la mradi huo, mwanzilishi wa Warriors from the East, Bwn. Lwanda Magere, amesema wanafunzi watakaopata ujuzi huo wanaweza kuutumia katika kutengeneza na kuuza vyombo, kupiga muziki au kuanzisha shughuli za kiuchumi zinazohusiana na sanaa.
Magere amesema mwanafunzi anayepata ujuzi huo anaweza kuutumia katika kupiga muziki, kutengeneza na kuuza vyombo au kuanzisha shughuli nyingine za kiuchumi zinazohusiana na sanaa.
“Tunaukaribisha sana mradi huu kwa sababu una nia ya kuwajenga watoto wetu wawe sehemu ya kizazi kitakacholinda na kuendeleza urithi wetu. Shule yetu inathamini sana elimu ya amali kwa sababu mtoto anahitaji pia kuwa na ujuzi unaoweza kumsaidia katika maisha yake.”
Kwa upande wake, Afisa Utamaduni wa Jiji la Arusha, Enock Philip, amesema uongozi wa Jiji kupitia Ofisi ya Mkurugenzi umeuwezesha mradi huo kwa kutoa vibali na kurahisisha upatikanaji wa shule zitakazofikiwa.
Naye Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Nile Blues, Renalda Masawe, amesema mafunzo hayo yatawapa wanafunzi ujuzi unaoweza kuwa chanzo cha ajira na kujiajiri.
“Mwanafunzi anaweza kujiajiri kupitia muziki. Anaweza kujifunza jinsi ya kutengeneza vyombo na akaviuza, akaanzisha hata gallery au akauze sokoni.”
Lengo ni kuhakikisha vyombo vya asili kama vinubi, zeze na nyatiti vinaendelea kurithiwa na kizazi kipya, huku wanafunzi wakitumia ujuzi huo kuhifadhi utamaduni na kujenga fursa za kiuchumi.
Mwisho.








Comments
Post a Comment