WADAU WA SEKTA YA ELIMU WATAKA MASOMO YA SANAA SHULENI, WATOTO WAPEWA ELIMU KWA VITENDO



Na Gladness Kowero Arusha.

Elimu ya nadharia pekee imeelezwa kuwa changamoto kwa wanafunzi katika kukuza ujuzi wa vitendo, huku wadau wa elimu wakihimiza kuwepo kwa programu zinazowawezesha watoto kujifunza kwa vitendo.

Akizungumza mara baada ya  mradi wa kuwafundisha wanafunzi kutengeneza na kutumia vyombo vya muziki kufika shuleni hapo, Mwalimu wa michezo shule ya msingi Arusha School Madamu Adeline Mollel amesema mafunzo hayo yamewasaidia watoto kuelewa zaidi kwa kuwa wamepata nafasi ya kuona na kufanya kile wanachojifunza.

“Changamoto kubwa ni kwamba mara nyingi tunapata elimu ya nadharia, lakini kwenye vitendo inakuwa changamoto. Mradi huu umewasaidia watoto kutoka kwenye nadharia na kujifunza moja kwa moja kwa vitendo.”
  



Mradi huo unaotekelezwa na Warriors from the East kupitia Nile Blues Project, umelenga kukuza vipaji na ubunifu wa wanafunzi, pamoja na kuwafundisha namna ya kutengeneza na kutumia vyombo vya muziki vya asili vilivyotumiwa na mababu zetu.

Kwa upande wake mmoja wa wadau wa mradi huo Bwn David Job Nafasi Art space ameiomba Serikali na wadau wa elimu kuendelea kuunga mkono programu za elimu ya vitendo, ikiwemo kuangalia uwezekano wa kuingiza masuala ya sanaa na utamaduni katika mtaala wa elimu.





Aidha, ameomba mradi huo ufikishwe katika shule nyingi zaidi ili kuwapa wanafunzi wengi fursa ya kujifunza, huku akisisitiza kuwa ujuzi huo unaweza kuwawezesha vijana kukuza vipaji vyao na kujiajiri.

Kwa upande mwingine, mradi huo umeelezwa kuwa ni sehemu ya jitihada za kuhifadhi utamaduni wa asili na kuwafanya watoto kuujua, kuuthamini na kuendeleza muziki na sanaa za kitamaduni.

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

WATUMISHI NGORONGORO KUNUFAIKA NA MILIONI 500, WAONYWA MIKOPO KAUSHA DAMU.

UGANDA ELECTION COMMISSION CONTINUES RECEIVING RESULTS AS MUSEVENI TAKES EARLY LEAD