WADAU WA SEKTA YA ELIMU WATAKA MASOMO YA SANAA SHULENI, WATOTO WAPEWA ELIMU KWA VITENDO
Na Gladness Kowero Arusha. Elimu ya nadharia pekee imeelezwa kuwa changamoto kwa wanafunzi katika kukuza ujuzi wa vitendo, huku wadau wa elimu wakihimiza kuwepo kwa programu zinazowawezesha watoto kujifunza kwa vitendo. Akizungumza mara baada ya mradi wa kuwafundisha wanafunzi kutengeneza na kutumia vyombo vya muziki kufika shuleni hapo, Mwalimu wa michezo shule ya msingi Arusha School Madamu Adeline Mollel amesema mafunzo hayo yamewasaidia watoto kuelewa zaidi kwa kuwa wamepata nafasi ya kuona na kufanya kile wanachojifunza. “Changamoto kubwa ni kwamba mara nyingi tunapata elimu ya nadharia, lakini kwenye vitendo inakuwa changamoto. Mradi huu umewasaidia watoto kutoka kwenye nadharia na kujifunza moja kwa moja kwa vitendo.” Mradi huo unaotekelezwa na Warriors from the East kupitia Nile Blues Project, umelenga kukuza vipaji na ubunifu wa wanafunzi, pamoja na kuwafundisha namna ya kutengeneza na kutumia vyombo vya muziki vya asili vilivyotumiwa na mababu zetu. Kwa u...